Nyimbo Standard Hymns Lyrics: "SALA YA ASUBUHI"
"Uwe radhi Bwana, hii siku ya leo utulinde na dhambi."
H.C.I [P.M]
Baba, Mwana, Roho, Mungu Mwenye enzi,
kila tukiamka tunakuabudu.
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi,
Ewe Utatu, tunakusifu.
Baba, Mwana, Roho, wakuaminio
Wanakutoalea, shukurani zao,
Wakusujudia malaika nao:
Wewe U mwanzo, nawe U mwisho.
Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani,
Utukufu wako haoni mkosa;
U mtakatifu, nawe U mapenzi,
U peke yako, mwenzio huna.
Baba, Mwana, Roho, Mungu Mwenye enzi,
Ulivyoviumba vyote vyakusifu:
Baba, Mwana, Roho, Mungu wamapenzi,
Ewe Utatu, tunakusifu.
********End********
The List 👇of Nyimbo Standard Hymns in Kiswahili;
2. "Awake, My Soul, and with the Sun". (2)
3. "O Jesus Lord of Heaven Grace." (3)
4. "The Morning Bright with Rosy Light." (4)
10. "My Father, I thank Thee For Sleep". (10)