Nyimbo Standard Hymns Lyrics: "SALA YA ASUBUHI"
S.S AND S. 482. [D. 6S.]
Nakushukuru Baba,
Kwa raha tulizi,
Nimehifadhiwa
Kwa wako ulinzi:
Nichunge kwa wema,
Hivi leo kutwa,
Salamani mwako,
Nipate jificha.
Nami nikupende
Upendaye wana
Mfano wa mimi.
Ndiwe Mwema, Bwana.
Nipe roho nzuri
Iliyotakata,
Uwe Mtulizi
Katika matata.
Nipe kupendeza
Kwa wakubwa wangu
Na kuwasikiza,
Liwe fungu langu;Uwape baraka,
Na rafiki wote,
Afya njema pia,
Walipo po-pote.
******END*****
The List 👇of Nyimbo Standard Hymns in Kiswahili;
1. "Holy, Holy, Holy, Lord God Almighty." (1)
2. "Awake, My Soul, and with the Sun". (2)
3. "O Jesus Lord of Heaven Grace." (3)
4. "The Morning Bright with Rosy Light." (4)
10. "My Father, I thank Thee For Sleep". (10)