8. "My God, is Any Hour So Sweet". (8)

Nyimbo Standard Hymns Lyrics: "SALA YA ASUBUHI"


H. C.  209. [8s. 4.]

Mungu ninakuja kwako,

Naitwa na neno lako,

Nije miguuni pako,

Asubuhi.


Nakukaribia wewe,

Daima nifurahiwe,

Lazima nisizuiwe,

Na dunia.


Naingia nyumba yako,

Sifai kuja uliko,

Ila ni mapenzi yako,

Kunivuta.


Nguvu na nirejezewe,

Dhambi na nisamehewe,

Kwako na nibarikiwe,

Hivi leo.


Moyo uliotakata,

Nguvu za kupiga vita,

Nihimizwe nikisita,

Bwana nipe.


Nisiwe nayo tashwishi,

Nguvu zangu hazitoshi,

Roho yangu itaishi,

Kwa imani.


Hata nifike mbinguni,

Sina tamu duniani,

Kama pako miguuni,

Bwana wangu.


********END********


  

The List 👇of Nyimbo Standard Hymns in Kiswahili;

Post a Comment

Previous Post Next Post