Nyimbo Standard Hymns Lyrics: "SALA YA ASUBUHI"
H. C. 243. [IIS.]
Mungu, Bwana wetu wa kutukuzwa,
Twakusifu wewe, wetu Mlinzi;
Kati ya mabaya yote ya giza,
Tumepata nguvu kwa usingizi.
Tukutumikie kwa nguvu hizi,
Na kutenda kazi zenye imani;
Tusiyaandame ya utelezi,
Ya dunia, mwili, na ya shetani.
Macho haya yetu yasitazame,
Masikio yetu yasisikize,
Wala ndani yetu, msiwe kamwe,
La kukukasiri. Bwana tutunze.
Mambo na maneno yetu ya leo,
Kwako yawe safi, matakatifu.
Kila tuazalo ndani ya myoyo,
Liwe la usafi, si la uchafu.
Baba, ukipenda, wema utupe,
Dhiki na mashaka tusiyaone:
Shukurani nayo iongezeke
Na tukae mwako, tusikosane.
***********END***********
The List 👇of Nyimbo Standard Hymns in Kiswahili;
1. "Holy, Holy, Holy, Lord God Almighty." (1)
2. "Awake, My Soul, and with the Sun". (2)
3. "O Jesus Lord of Heaven Grace." (3)
4. "The Morning Bright with Rosy Light." (4)
10. "My Father, I thank Thee For Sleep". (10)