Nyimbo Standard Hymns Lyrics: "SALA YA ASUBUHI".
Mbingu,kukipambauka,
Zina rangi nzuri;
Kila siku nuru zake
Kwetu hunawiri;
Na wekundu wa jioni
Hutufurahisha:
Uzuri huo lakini
Wendelea kwisha.
Ingawa hatuyaoni
Hayo ya mbinguni,
Malango ya lulu safi
Yasiyo ya chini;
Njia zake za dhahabu
Zinavyotengezwa;
Jua-la-haki halitwi,
Mwenye kusifiwa.
Tumaini la dunia
Huzimika huku,
Nguo zao watu wema
Zinavyo vipaku;
Myoyo isiyo na dhambi,
Iliyotakata,
Tutaipata mbinguni,
Tuimbe daima.
Hata tunayo imani,
Na matumaini;
Na neema tumepewa,
Tufike mbinguni:
Twendako kuna amani
Isiyo ya kwisha,
Na ukamilifu wote
Wa kufurahisha.
Bwana, kwa mapenzi yako
Na mateso pia,
Uhai uliotoa
Kwa hii dunia,
Tusikose wema wako
Huo wa mbinguni;
Wala, kwa dhambi za hapa,
Tusikose taji.
******END*******